ISIMU

Wanaisimu wanachunguza historia ya ginsi majamii ya kilugha yameyakalia maeneo ya mashariki mwa Bonde kubwa la Congo, wakitilia hasa mkazo juu ya kusambaa Wabantu, uhusiano wa lugha zao, baadaye, na pia historia kuhusu orodha ya makabila ya kibantu yanayopatikana kandokando mwa mito.

Katikati ya mashariki mwa Bonde kubwa la Congo, karibu sana na kaskazini ya maporoko, pale mto Lualaba unageuka kuwa jito Congo, ndipo panapatikana Kisangani. Ni mji wa tatu wa RDC. Mji huu na kandokando zake ni kabisa njia panda ya makundi madogo ya lugha za kibantu (Congo Basin/ouest ; central/est, Boan ( ?), Lebonya ( ?)) na vilevile lugha moja ya kiubangui (mba). Mbali kidogo, eneo hili ni tofauti kabisa. Kunapatikana, magaribi mwake, kundi moja ndogo la lugha za kibantu (Congo Rivers), na kaskazini kundi lingine la lugha za kiubangui, na katika sehemu ya kaskazini-mashariki mwa Bonde kubwa la Congo, kuna pia lugha za kisudani ya kati na vilevile makabila ya wawindaji-wachumaji ambao inahadisiwa kama wameacha, hapo zamani, kutumia lugha zao za asili.Wanaisimu, katika mradi BANTURIVERS, wanajifunza ni ginsi gani njia panda hii ya lugha iliweza kuanza : ni majamii gani yalikuwepo mwanzo, yalitokea wapi, ni wakati gani yaliweza kukutana na, baada yake, mabadilishano yao yalikuwa ya aina gani. Zaidi ya hayo wanaisimu watachunguza historia kuhusu moja ya sababu zisizokuwa za kilugha ambayo iliweza kuwavuta ao kurahisisha watu hawa kuishi katika mazingira haya, kwa mfano ginsi yao ya kutumikisha mali za majini.

Mradi BANTURIVERS unashurlika hasa na kusambaa kwa Wabantu katika eneo la mashariki mwa Bonde kubwa la Congo. Mipangilio ya sasa ya lugha inaeleza historia nyingi kuhusu eneo hili. Bastin et ali.( 1999) wanafikiria ya kama ni lugha za « kiboa » na « lebonya » ambazo zilifika za kwanza kwenye eneo hili. Lugha za kibantu za sehemu za magaribi na zile za mashariki zilifika tu baadaye. Katika moja ya mipangilio mingine, Grollemund et al.( 2015), wanafikiria ya kwamba lugha ya kiboa na ile ya lebonya zimefika katika eneo hili pamoja na lugha za « Central-Western Bantu ».Wazo hili linabadilisha kabisa historia ya eneo hili. Wanaisimu watapendekeza mpangilio mpya wa lugha utakaotegemea sifa za kimaneno na zile za kisarufi wakitumia njia ya ginsi makabila yamepata kuzaliwa na pia wakitegemea, kwa utaratibu sana, isimu linganishi. Mpangilio huu mpya wa lugha utawezesha kuyatambua majamii ya kilugha kihistoria pamoja na njia walizozifwata mpaka kufikia kwenye eneo la Bonde kubwa la Congo. Hatua ya pili inayotiliwa mkazo katika utafiti huu itaelekea mahusiano mfululizo kati ya lugha husika na lugha nyingine mnamo eneo hili : mabadilishano ya maneno na mambo mengine ya kilugha, na hata uwezekano wa kutambua sifa za kale na za msingi za lugha.

Zaidi ya hayo, wanaisimu wanachunguza pia upande wa historia ya mito. Kwa kupitia njia ya maneno na vitu, hasa ile ya isimu linganishi kuhusu maneno ya kiutamaduni, historia ya orodha ya makabila ya Wabantu kandokando mwa mito inaweza kujifunzwa: ni aina gani ya mito majamii ya zamani ya Wabantu yaliijua ? Ni ginsi gani walitumia mito hii : kwa uchukuzi na kwa kujipatia chakula ? Wanaisimu watachunguza pia mada kuhusu usafiri kwenye mito, uvuvi na mapishi ya samaki ; na tena maswali ya tamaduni za kijamii kuhusu mito na maisha kandokando ya mito, biashara na jiografia ya vijiji pamoja na kazi zilizofanyiwa kandokando mwa mito. Tafiti za kiisimu zitajulisha ni aina gani za ujuzi makabila haya yalikuwa nazo kabla ya kufika kwao kunako eneo la mashariki mwa Bonde kubwa la Congo ; na ni ujuzi gani makabila haya yaliweza kupata katika mahusiano yao, baada ya myaka, ya karne juu ya kugeuka maarufu. Matokeo ya tafiti hizi yatachangia katika fikra kuhusu sababu sisizokuwa za kilugha juu ya kusambaa kwa Wabantu.

Wanaisimu wa mradi BANTURIVERS wanachangia pia katika kuandika lugha zinazokuwa mashariki mwa Bonde kubwa la Congo. Lugha nyingi za eneo hili hazijapata kuandikwa vema ao zimejifunzwa tu kijuujuuu. Kinyume ni kwamba wanaisimu wanabidi kukusanya data wanapopatikana kwenye eneo hili. Kutokana na hatari mnamo kuwa lugha hizi, uwanja wa isimu utaleta maelezo kuhusu hali ya sasa ya lugha husika.

Références

Bastin, Yvonne, André Coupez & Michael Mann. 1999. Continuity and Divergence in the Bantu Languages: perspectives from a lexicostatistic study. Tervuren: Musée Royal de l’Afrique Centrale.

Grollemund, Rebecca, Simon Branford, Koen Bostoen, Andrew Meade, Chris Venditti & Mark Pagel. 2015. Bantu expansion shows that habitat alters the route and pace of human dispersals. Proceedings of the National Academy of Sciences (PNAS).