ANTHROPOLOJIA

Sifa moja ya pekee ya mradi BANTURIVERS ni kuingiza anthropolojia katika tafiti za kihistoria. BANTURIVERS inafanya nguvu ya kutia sibitisho za kisasa katika mazingira ya siku hizi juu ya kutabiri vizuri zaidi nyakati zilizopita. Wanaanthropolojia wanaleta maelezo kuhusu majamii mawili ya wavuvi, mfumo wao juu ya kazi za kujipatia chakula, mitandao ya kibiashara na mtazamo wao wa maisha katika kandokando mwa mito. 

Hata kama BANTURIVERS inahusika na nyakati za kale za mbele ya kipindi cha Ukoloni, mradi huu unategemea data za nyakati za sasa, yaani zile za karne mbili za mwisho. Hii ni kweli hasa kwa upande wa isimu ambayo inatumika na maandishi ya tangu mwisho wa karne ya 19. Ni kweli, vilevile, kwa tafiti za kiarkeolojia ; kwa mfano, katika kujifunza desturi za ufinyanzi wa vyombo siku hizi. Ikiwa kama lugha pamoja na utamaduni wa kivyombo wa siku hizi ni msingi wa tafiti za kihistoria, inaonekana wazi ya kwamba mazingira ya kiethnografia ambamo vinapatikana yangelibidi kujifunzwa na kuchambuliwa vizuri. Pahali pa kutegemea maandishi ya kiethnografia ambayo, siku hizi, ni haba na yenye kupitwa na wakati, watafiti wa BANTURIVERS walijiunga na wanaarkeolojia juu ya kujifunza ukweli wa sasa wa mada za tafiti za mradi katika majamii fulani ya Bonde kubwa la Congo. Wanaanthropolojia wanaangalia mbinu za kujipatia chakula na kazi ya uvuvi, mifumo ya kubadilishana vitu na /ao ya kibiashara, na pia jiografia ya kazi za kupata chakula katika vijiji vinavyopatikana pembeni ya mito.

Kuhusu ginsi ya kujipatia chakula, eneo la mashariki mwa Bonde kubwa la Congo ni nzuri sana kwa sababu majamii fulani yamejipatia umaarufu wa pekee na yanafanya biashara na majamii mengine maarufu katika mbinu tofauti. Katika eneo la mashariki mwa msitu wa Ikweta , katika Afrika ya kati, kunajulikana kuweko mifano mingi ya mbinu zinazotegemeana juu ya kujipatia chakula. Mahusiano ya kutegemeana kati ya Wambuti wawindaji –wachumaji na majamii jirani ya walimaji yameelezewa kwa namna ya pekee, hasa zaidi kwa sababu mahusiano haya yanaonekana kuweko pia katika lugha zinazotumiwa na majamii ya Wambuti (cf.Terashima 1986, 1998). Hunt (1999 :17, 36) anachunguza mfumo wa mabadilishano ya vitu uliokuwepo tangu mnamo mwisho wa karne ya 19 kati ya wavuvi Walokole na mabingwa wa msitu Bambole. Ankei (1984), kwa upande wake, anajifunza jambo lingine nzuri sana linaloonesha wazi ya kwamba kupata umaarufu katika mbinu fulani juu ya kujipatia chakula hakuambatani na kabila ao lugha fulani, sababu mnamo myaka ya 1970, kandokando mwa Lualaba, watu fulani waliojitambulisha kama « Wasongola » walikuwa wakizungumza lugha ya kisongola ao ile ya kiombo. Lugha hizi zimepangwa katika makundi madogo tofauti ya lugha za kibantu. Watu wengi kati yao waliishi kwa kilimo. Lakini kundi moja lilikuwa na sifa ya pekee katika uvuvi : Waenya ao Wasongola-Enya . Jina hili linakumbusha lile la wavuvi wanaopatikana katika sehemu ya chini ya mto Lualaba. Zaidi ya hayo, Waenya hawa walizungumza lugha ya kisongola ao kiombo. Basi, Wasongola-Enya walijitambulisha katika makundi mawili tofauti. Na wengine kati yao walizungumza lugha moja isiyohusiana hata kidogo na moja ya makundi yale mawili. Wanaanthropolojia wa mradi BANTURIVERS wanaelezea kuhusu majamii yaliyogeuka maarufu katika uvuvi hivi sasa na ginsi yaliweza kuingia katika mitandao ya kibiashara kwenye maeneo haya.

Tafiti za kiarkeolojia zinachunguza pia maswali ya utamaduni wa kijamii juu ya maisha kandokando mwa mito, kwa mfano ni ginsi gani jamii linatumia udongo, mahusiano kati ya watu wanaoishi juu na wale wanaoishi chini ya mto, mahusiano na watu wanaokaa kwenye maeneo ya ndani, mahusiano kati ya wavuvi, makabila yanayo kuwa na desturi ya kuunguza pori kabla ya kulima na makabila ya wawindaji-wachumaji, kati ya watumwa na pembe ( cf. Harms 1981), na mahusiano kati ya makundi madogo ya kiroho na nguvu zinazoambatana na mito.

Uwanja wa kianthropolojia unajishurlisha, kwa uchache, na majamii mawili ya wavuvi yanayoishi katika sehemu mbalimbali za eneo la mashariki mwa Bonde kubwa la Congo. Mbinu zao kwa kujipatia mali kutoka kwenye mito zitalinganishwa, vilevile matumizi yao, kwa namna ya pekee, ya udongo, mitandao yao ya kibiashara na ginsi ulimwengu wao wa kiroho na ule wa alama zinaambatanishwa na mito.

Références

Ankei, Yuji. 1984. Fish as “primitive money”: Barter markets of the Songola. Senri Ethnological Studies 15. pp. 1–68.

Harms, Robert W. 1981. River of wealth, river of sorrow. The central Zaire basin in the era of the slave and ivory trade, 1500-1891. New Haven and London: Yale University Press.

Hunt, Nancy Rose. 1999. A Colonial Lexicon. Of Birth Ritual, Medicalization, and Mobility in the Congo. Durham: Duke University Press.

Terashima, H. 1986. Economic exchange and the symbiotic relationship between the Mbuti (Efe) Pygmies and the neighboring farmers. Sprache und Geschichte in Afrika, 7(1), 391–405.

― 1998. Honey and holidays: The interactions mediated by honey between the Efe hunter-gatherers and the Lese farmers in the Ituri forest. African Study Monographs Supplementary Issue, 25: 123–134.