ARKEOLOJIA

Wanaarkeolojia wanatoa sibitisho za moja kwa moja ya kukaliwa na watu eneo la mashariki mwa Bonde kubwa la Congo kwa kupitia masalio ya vitu, na kwa kulinganisha utamaduni wa kivyombo wa sasa na ule wa zamani, na pia kwa njia ya mahojiano na wafundi wa siku hizi.

Hadi hivi karibuni, eneo la kandonkando mwa Kisangani lilikuwa wazi kwenye ramani ya kiarkeolojia ya RDC. Masalio ya mradi River Connaissance (Eggert 1987, 1992 miongoni mwa vitabu ; Wotzka, 1995) yanapatikana hasa kunako sehemu ya magaribi, ndani ya Bonde kubwa la Congo, pembeni ya mito inayolipatia maji jito Congo, kati ya ziwa Tumba na mto Lulonga. Lakini maeneo ya Mercader yanapatikana hasa kwenye sehemu za kaskazini-magaribi, kaskazini mwa Epulu (Mercader 2003). Data pekee kuhusu eneo la mashariki mwa Bonde kubwa la Congo zimetolewa na wanaarkeolojia wa jopo la BANTURIVERS wakati wa uchunguzi wao mnamo myaka ya 2010 na 2013. Maeneo yaliyopekuliwa yanaonesha kuweko vijiji katika sehemu ya Aruwimi, pale Lomami na Lindi, kati ya myaka 2200 na 1900 BP. Uchambuzi wa ufinyanzi wa vyungu unaonesha kuweko aina tofauti za utengenezaji wa vyungu, ikiwemo aina moja ambayo asili zake zinaoenekana kuwa ni maeneo ya Saheli (Livingstone-Smith et al. 2016). Matokeo ya mwanzo yanaleta matumaini kuhusu uvumbuzi wa hali ya nyakati za kale za njia panda ya sasa ya kiutamaduni.

Lengo la kwanza la sehemu ya arkeolojia, katika mradi huu, ni kutoa sibitisho za kihistoria za moja kwa moja kuhusu kukaliwa na watu eneo hili. Kutokana na hali za utunzaji vitu katika maeneo yaliyopekuliwa, inawezekana hata kupata sibitisho za moja kwa moja kuhusu mbinu za kujipatia chakula hapo zamani, kama vile mbinu juu ya matumizi ya mito. Wanaarkeolojia wataunda utaratibu wa kupanga myaka na matukio pamoja na utaratibu wa utamaduni wa majamii yanayoishi siku hizi katika msitu wa Ikweta. Kutokana na matatizo ya kutunza vitu katika udongo wenye asidi ndani ya msitu, arkeolojia inashurlika hasa na vipande vya vyungu na vyombo vingine vilivyofinyangwa, pia na vile vilivyotengenezwa kwa mawe ao na sehemu tu zilizobakia baada ya kutengenezwa kwao. Njia ya nguvu zaidi ya uchunguzi inaelekezwa kwenye mito. Na hata kama njia hii inaweza kusababisha matatizo fulani juu ya kutambua ni watu gani waliokaa kwenye maeneo ya kandokando ya mito, imeonesha ubora wake katika kugundua mimea mingi inayosongana pembeni ya mito, ndani ya msitu wa Ikweta. Uchunguzi wa maeneo makubwa zaidi ndani ya Bonde kubwa la Congo umeonesha uwezekano wa kujenga upya ginsi maeneo haya yaliweza kukaliwa na watu mnamo myaka 2500 iliyopita. (Wotzka 1995 ; Eggert 2014). Njia hii ilitumiwa kwa manufaa sana kaskazini-mashariki mwa jito Congo, zikiwemo sehemu za chini za mito inayolipatia maji jito Congo (Livingstone-Smith et al. 2016).

Ya pili, data za kisasa zitakusanywa juu ya kujifunza mbinu za ufinyanzi wa vyungu, mabadilishano ya vitu, na mitandao ya hapo zamani na ya sasa. Mahojiano na wanawake watengenezaji wa vyungu yataleta maelezo zaidi kuhusu ile ilikuwa njia ya uendeshaji kazi, upande wa kijamii wa kazi yao, na ule wa habari. Si rahisi kupata maelezo haya kuhusu vyungu vilivyofukuliwa na vinavyotoa alama za wafundi na mitandao iliyovitengenezesha.

Références

Eggert, Manfred K.H. 1987. Archäologische Forschungen im zentralafrikanischen Regenwald. In: Portner, R. & Niemeyer, H.G. (eds.). Die großen Abenteuer der Archäologie, Band 9. Salzburg: Andreas Verlag, pp. 3217-3240.

―. 1992. The Central African Rain Forest: Historical Speculation and Archaeological Facts. World Archaeology Vol. 24 (1): 1-24.

― 2014. The archaeology of the Central African rainforest: Its current state. In: Renfrew, C. & Bahn, P. (Eds). The Cambridge World Prehistory (1). New York: Cambridge University Press. pp. 183–203.

Livingstone-Smith, A., Cornelissen, E., de Franquen, C., Nikis, N., Mees, F., Tshibamba Mukendi, J., Beeckman, H., Bourland, N. & Hubau, W. 2016. Forests and Rivers: The Archaeology of the North Eastern Congo. Quaternary International.

Mercader, J. 2003. Foragers of the Congo. The early settlement of the Ituri Forest. In: Mercader, J. (ed.). Under the Canopy. New Brunswick: Rutgers University Press. pp. 93-116.